Beki kisiki wa Simba Paschal Wawa amesema hawawezi kuanza kuwaza ubingwa sasa wakati bado wana mechi nyingi za kucheza
Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli Fc juzi, Simba imejiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 56 ikiongoza kwa tofauti ya alama 12 dhidi ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili na alama 17 dhidi ya Yanga inayoshika nafasi ya tatu
Wawa amesema wachezaji wamejipa kazi ya kuhakikisha wanashinda mechi zao zote, hivyo kwa sasa hawawezi kuwaza ubingwa kwa kuwa kazi hiyo bado hawajaimaliza
"Tunafahamu tuna kazi ya kutetea ubingwa ila kwa sasa hatuwezi kusema sisi ni mabingwa tayari, bado tuna mechi nyingi za kucheza na ushindani ni mkubwa. Kupitia matokeo mazuri tutakayopata uwanjani yatafungua njia kwetu kupata kile tunachokihitaji," amesema
"Ili kutimiza lengo hilo, kama wachezaji tumejipa kazi ya kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kwa kila mchezo unaokuja mbele yetu"
Simba imerejea jijini Dar es salaam jana ambapo kesho Jumanne itawakaribisha Kagera Sugar kwenye mchezo mwingine wa ligi kuu ambao utapigwa uwanja wa Taifa