Baada ya kuibuka na ushindi kwenye mechi mbili zilizopita, mashabiki wa klabu ya Simba wametakiwa kuwa na imani na benchi la ufundi linaloongozwa na Sevn Vandenbroeck
Kabla ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, Simba haikuwa kwenye kiwango bora kwa takribani mechi tatu mfululizo jambo lilolopelekea mashabiki kushinikiza uongozi kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi
Hata hivyo kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar na Lipuli Fc Simba imeonekana kurejea kwenye kiwango chake
Mkufunzi wa zamani wa timu hiyo Jamhuri Kiwhelo amesema wakati mwingine mashabiki kukosa uvumilvu husababisha presha isiyo ya lazima kwa wachezaji, benchi la ufundi na uongozi
Julio amesema ana imani kubwa na kocha Vandenbroeck, muhimu apewe muda ili aweze kutengeneza timu yake
“Mashabiki na wanachama wa Simba wanatakiwa kumpa muda kocha Sven, kwa sababu kwa muda aliokaa klabuni hapo ni ngumu wachezaji kushika falsafa yake, ni ngumu sana kocha mpya anapokwenda kwenye timu mpya, halafu mbinu zake zikakubali kwa haraka, hivyo apewe muda tu atafanya vizuri kwa kuwa anaonekana ni kocha mzuri,” amesema.
Kwenye michezo ya nyuma Sven alikuwa akitumia mfumo wa 4-3-3 akiweka mshambuliaji mmoja mbele
Hata hivyo tangu mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar Sven anatumia 4-4-2, akiweka washambuliaji wawili mbele, John Bocco na Meddie Kagere
Ni mfumo ambao umeipa Simba mafanikio katika mechi mbili zilizopita
Pengine ataendelea kuutumia kwenye mechi nyinine zinazokuja