Pamoja na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli Fc kwenye mchezo wa ligi kuu jana, kocha mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck hakufurahishwa na mazingira ya uwanja wa CCM Sokone
Mvua ilisababisha uwanja huo kujaa tope hivyo kuinyima Simba fursa ya kucheza kandanda lao la kuvutia
Sven amesema pengine atahitaji kuwanunulia wachezaji wake viatu maalum kwa ajili ya kukabiliana na mechi zinazochezwa kwenye mazingira ya viwananja 'vikorofi'
"Nilifurahishwa na wachezaji wangu jinsi walivyocheza pamoja na kuwa uwanja haukuwa rafiki kwetu. Pengine itabidi niwatafutie wachezaji wangu viatu vyenye meno marefu ili wasipate shida wanapocheza mazingira ya viwanja vyenye tope na utelezi," alisema
"Tulilazimika kufanya kazi kama timu kwa muda wote wa mchezo kwa kuwa hatukuwa na nafasi ya kucheza mchezo wetu wa siku zote"
Bao la John Bocco liliihakikishia Simba ushindi muhimu ambao umeendelea kuwakita kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 56