Bao lililofungwa na nahodha wa Simba John Bocco, limeihakikishia timu hiyo kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Samora leo
Bocco ambaye alikuwa nje ya kikosi cha Simba kwa muda mrefu, ameendelea kuimarika sasa akifunga kwenye mchezo wa pili mfululizo
Alifunga moja ya mabao ya Simba kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo uliopita

Tangu amrejee dimbani tayari ameifungia Simba mabao matatu
Bocco ameendelea kufanya kazi hiyo wakati mshambuliaji kinara wa mabao Meddie Kagere akiwa amepunguza kasi ya kufunga
Kagere sasa hajafunga kwenye mchezo wa tano mfululizo
Lakini pamoja na kutokufunga, Kagere amekuwa na mchango mkubwa kwa kutoa pasi za mabao
Amefunga mabao 12 na kutoa pasi sita za mabao hivo kumfanya awe amehusika kwenye mabao 18 ya Simba