Wakati washindani wake Azam Fc na Yanga wakishindwa kupatga ushindi kwenye michezo yao ya ligi iliyopigwa leo, Simba imeendelea kujisafishia njia kuelekea ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa tatu mfululizo baada ya kuichapa Lipuli Fc bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Samora mapema leo
Bao pekee la ushindi la Simba lilifungwa na nahodha John Bocco ambaye ameendelea kuimarika baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa muda mrefu
Ushindi huo umeifanya Simba ifikishe alama 56 na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi
Azam Fc inayoshika nafasi ya pili, ilichapwa na Coastal Union mabao 2-1 hivyo kubaki na alama 44 wakiachwa na Simba kwa tofauti ya alama 12
Yanga nayo ikalazimishwa suluhu ya bila kufungana wakifikisha alama 39, wana deni la alama 17 kwa Simba
Mchezo unaofuata ni dhidi ya Kagera Sugar na utapigwa Februari 19 2020 kwenye uwanja wa Taifa