Ambulance yaiponza Ruvu Shooting, yapokwa alama tatu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Feb 2020
Ambulance yaiponza Ruvu Shooting, yapokwa alama tatu

Maamuzi mengine ya kikao cha kamati ya Saa 72 kilichoketi mwanzoni mwa wiki huu

Mechi namba 205 ; Ruvu Shooting vs Tanzania Prisons FC.

Tanzania Prisons FC imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu kwenye mchezo uliokuwa ufanyike Februari 11, 2020 baada ya timu ya Ruvu Shooting FC ambayo ndiyo timu mwenyeji kushindwa kuleta gari la wagonjwa (Ambulance) uwanjani kama Kanuni ya 14 (2l) inavyosema na kusababisha mchezo kuvunjwa na mwamuzi baada ya kusubiri kwa dakika 30 bila gari hiyo kutokea

Mechi namba 200 ;  Ruvu Shooting 0 FC vs Yanga SC 1

Timu ya Yanga SC imepewa Onyo kali kwa kosa la kuwakilishwa na watu pungufu ya idadi inayotakiwa katika kikao cha maandalizi ya mechi (Pre-match meeting) na kujaza jina la Kocha wa walinda milango Peter Manyika kuwa amehudhuria kikao hicho wakati hajahudhuria .Kitendo hicho kilifanyika katika maandalizi ya mchezo uliofanyika February 08, 2020 katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam

Mechi namba 197 ; Singida United FC 2-2 Mwadui FC

Mchezaji wa Mwadui Hashim Yahya Mussa amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kwa kosa la kuwaonyeshea kidole cha kati watazamaji kama ishara ya matusi baada ya filimbi ya kumaliza mchezo ilipopigwa kitendo hicho kilifanyika katika mchezo uliofanyika February 8, 2020 katika uwanja wa Namfua mjini Singida

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
51m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’