Mfumo wa 4-4-2 utarudisha mabao ya Kagere

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Feb 2020
Mfumo wa 4-4-2 utarudisha mabao ya Kagere

Baada ya mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, kuonekana amepunguza kasi katika upachikaji wa mabao, mabadiliko ya mfumo wa uchezaji yanaweza kumrejesha Mnyarwanda huyo kwenye ubora wake wa kuzifumania nyavu

Licha ya Kagere kuongoza katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na mabao 12, lakini kasi yake ya kufunga imepungua tofauti na msimu uliopita aliochukua kiatu cha dhahabu kwa kutupia mabao 23.

Baada ya Aussems kuondoshwa kocha mpya Sven Vandenbroeck alikuja na mfumo tofauti ambapo amekuwa akitumia kuchezesha mshambuliaji mmoja mbele, jambo lililomfanya atumie viungo wengi

Baada  ya kubaini mapungufu, Sven amerejesha mfumo wa kuwatumia washambuliaji wawili mbele na sasa Kagere atakuwa anasimama na John Bocco.

Mfumo wa kuchezesha washambuliaji wawili ulianza kumpa matunda mazuri katika  mchezo uliopita ambao walishinda mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Katika mchezo huo, Bocco ndiye alifunga bao la kwanza kutokana na kazi nzuri aliyofanya Kagere

Sven amekiri kuwa mfumo wa 4:4:2 alioanza kuutumia kwa kumwanzisha Kagere na Bocco pamoja umekuwa na mafanikio.

"Pacha ya Bocco na Kagere wakicheza  pamoja inafanya timu kuwa na uwezo mkubwa wa kupeleka mashambulizi mbele, nina imani tutafunga mabao mengi zaidi kama itaendelea hivi," alisema.

Washambuliaji hao huenda wakaongoza safu ya ushambuliaji kwenye mchezo wa ligi kuu kesho dhidi ya Lipuli Fc ambao utapigwa uwanja wa Samora mkoani Iringa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’