Mabingwa wa nchi Simba waliwasili mkoani Iringa jana tayari kuwakabili Lipuli Fc 'Wanapaluhengo' kwenye mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa uwanja wa Samora
Baada ya kutua jana, jioni kikosi cha kocha Sven Vandenbroeck kilifanya mazoezi yake ya kwanza kwenye uwanja huo
Wakazi wa mkoa wa Iringa na maeneo ya jirani wametakiwa kukaa tayari kupokea burudani kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo ambao utapigwa hapo kesho
ADVERTISE HERE