Makocha wa Simba Sven Vandenbroeck na Selemani Matola wanaonekana kuwa na furaha baada ya juzi kuiongoza Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar
Inaelezwa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba iliwakalisha chini makocha hao na kuwataka wamalize tofauti zao (kama zipo) lakini muhimu kurejesha furaha ya mashabiki kwa kuhakikisha timu inacheza vizuri

Ushindi mnono uliopatikana juzi ni ishara kuwa wawili hao sasa wameuwasha moto
Keshokutwa Jumamosi wataiongoza Simba kwenye mchezo mwingine wa ligi dhidi ya LIpuli Fc, timu iliyowahi kufundishwa na Matola


ADVERTISE HERE