Simba tunampenda Ndemla, lakini hatumuoni uwanjani

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Feb 2020
Simba tunampenda Ndemla, lakini hatumuoni uwanjani

Ukizungumzia wachezaji ambao wanaiva sana na mashabiki wa Simba, kiungo Said Khamis Ndemla ni miongoni mwao

Kiungo huyu amekuwa kwenye kikosi cha mabingwa hao wa nchi kwa takribani miaka saba

Hata hivyo ni kama hana bahati ya kuaminiwa na makocha wote wanaopita Msimbazi

Pengine wakati wa kocha Pierre Lechantre na Masudi Djuma ndio alipata muda zaidi wa kucheza kwenye kikosi cha kwanza

Lakini tangu wakati huo amekuwa hana mwendelezo mzuri kwa makocha wengine waliopita Simba akiwemo wa sasa Sven Vandenbroeck

Mwanzoni Sven alionekana kumkubali sana Ndemla lakini imekuwa nadra sana kumuona uwanjani

Kuna wakati msimu uliopita alikwenda Sweden kufanya majaribio katika moja ya timu inayoshiriki ligi daraja la kwanza

Ilielezwa kuwa alifanikiwa kufuzu majaribio hayo lakini haijafahamika kilichomkwamisha kwenda Sweden

Hiki ni kipaji kikubwa sana ambacho kinaweza kupotea, ni vyema benchi la ufundi Simba likafanyia kazi mapungufu wanayoyaona kwake ili angalau wamsaidie kulinda kipaji chake

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’