Baada ya kuichabanga mtibwa Sugar mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Jamhuri jana, Simba mabingwa wa nchi wamepania kuendeleza moto huo mpaka mwishoni mwa msimu
Wakiwa kileleni mwa msimamo kwa tofauti ya alama tisa baada ya kufikisha alama 53, Simba inaelekea mkoani Iringa kuifuata Lipuli Fc
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema ushindi waliopata jana umeongeza ari na morali ya wachezaji na wamepania kuendeleza mwenendo huo kwenye mchezo utakaopigwa Februari 15
"Ushindi ni matokeo tuliyoyahitaji sana hasa baada ya kupoteza mchezo uliopita. Lengo letu ni kutetea ubingwa wetu hivyo matokeo haya yanatuweka salama"
"Hatuwezi kubweteka kwani bado kuna mechi nyingi lakini tutahakikisha tunapata matokeo kwenye kila mchezo iliyobaki tuweze kutetea ubingwa"