Sven asifu kiwango Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Feb 2020
Sven asifu kiwango Simba

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema vijana wake walistahili ushindi kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar kwani walikuwa bora kila idara

Aidha Sven amewasifu washambuliaji wake John Bocco na Meddie Kagere kuwa uwepo wao dimbani uliwarahisishia ushindi huo

"Wachezaji wangu walipambana tangu dakika ya kwanza, nadhani umeona jinsi kila mmoja alivyokuwa na shauku kuhakikisha tunashinda leo (jana). Tuliwachanganya Mtibwa Sugar kwa kubadili mfumo wetu wa uchezaji, umeona faida tuliyopa kwa kuwatumia John Bocco na Meddie Kagere," amesema

"Wakati mwingine unahitaji vikwazo ili uweze kujiimarisha. Matokeo ya mchezo uliopita yalitupa nguvu zaidi na nadhani sote tunafahamu lengo letu msimu huu, tunahitaji kutetea ubingwa"

Sven jana alirejea kwenye mfumo wa 4-4-2 akiwatumia Bocco na Kagere pamoja

Bocco ndiye aliyefunga bao la kwanza la Simba huku mengine mawili yakifungwa na Mohammed Hussein na Hassan Dilunga na kuihakikishia Simba ushindi muhimu wa mabao 3-0

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’