Leo mlinda lango Aishi Manula amerejeshwa kweye kikosi cha kwanza baada ya kukosekana kwa zaidi ya mwezi mzima majukumu yake yakisimamiwa na Beno Kakolanya
Baada ya Simba kuruhusu mabao manne kwenye michezo mitatu iliyopita, leo mabingwa hao wa nchi wametoka salama bila kuruhusu bao wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar
Manula ameonyesha kiwango kizuri leo kwani aliokoa mashambulizi kadhaa ya hatari yaliyokuwa yanaelekea langoni
Kiwango alichoonyesha leo kinaweza kumrejesha kwenye kikosi cha kwanza katika mechi zijazo pia
ADVERTISE HERE