Mtibwa Sugar vs Simba, lazima kieleweke uwanja wa Jamhuri leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Feb 2020
Mtibwa Sugar vs Simba, lazima kieleweke uwanja wa Jamhuri leo

Mabingwa wa nchi Simba leo wako mkoani Morogoro kuwakabili wana tamtam wa Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa uwanja wa Jamhuri

Huu ni mchezo muhimu sana kwa Simba pengine kuliko wapinzani wao Mtibwa Sugar licha ya kuwa nao wako katika presha ya kupata matokeo baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo

Jana kocha mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck alibainisha waziwazi kuwa leo wanahitaji kupata ushindi bila ya kujali mazingira yoyote watakayokutana nayo

Matokeo ya kufungwa bao 1-0 na JKT Tanzania hayakuwafurahisha Wanamsimbazi, hivyo leo hakuna matokeo mengine ambayo yanaweza kurejesha amani ya mashabiki zaidi ya ushindi

Msemaji wa Simba Haji Manara amewahasisha wachezaji kuwa leo wafahamu umuhimu wa kupata matokeo mkoani Morogoro

"Najua mnajua nini Wanasimba wanataka leo?. Najua mnajua Washabiki wetu watakuwa ktk hali gani jioni ya leo bila ushindi!!
Najua mnajua msingetamani nife au niumwe kisa matokeo mabovu leo. Mimi na Wanasimba wote tunawaamini na tunajua mkipambana hakuna wa kuwafunga nyie"

"Tuleteeni pointi tatu leo, nendeni kachezeni kwa spirit kubwa ili mwishoe tuondoke vinara uwanjani!!
Mungu wabariki Wafalme Simba, Mungu wape nguvu Machampioni wa nchi, wape na Maarifa wachezaji wetu wapendwa Insha'Allah"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
21h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’