Kocha wa zamani na Mwanachama maarufu wa Simba Jamhuri Kiwhelo 'Julio' amesema haamini kama tatizo la klabu ya Simba ni kocha
Julio amesema kocha Sven Vandenbroeck anapaswa kupewa muda kwani miezi miwili haitoshi kumuhukumu
Aidha, Julio amesema changamoto kubwa ambayo inaikabili klabu ya Simba sasa ni wachezaji kushuka viwango huku wengine umri ukiwa umewatupa mkono
"Kocha amekaa na timu miezi miwili tu, ni muda mchache sana kwa Mwalimu kuhukumiwa. Simba ina matatizo zaidi ya kocha, viwango vya wachezaji vimeshuka, wengine ni wazee mchango wao umekuwa ukipungua siku hadi siku," amesema
"Kumuondoa kocha haiwezi kuwa suluhu, apewe muda lakini wakati huo viongozi watatue matatizo ya msingi"
ADVERTISE HERE