Beki Yusufu Mlipili ni miongoni mwa wachezaji wa Simba waliosafiri leo kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar
Jina la Mlipili limetawala kwenye midomo ya mashabiki wa Simba siku za karibuni wakitaka aanzishwe kwenye kikosi cha kwanza
Baada ya Erasto Nyoni kuumia, Mkufunzi wa Simba Sven Vandenbroeck amekuwa akiwatumia Paschal Wawa, Kennedy Juma na Tairone Da Silva huku Mlipili akiwa hajacheza mchezo wowote wa kimashindano msimu huu
Huenda akapewa nafasi kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa Jumanne katika uwanja wa Jamhuri
ADVERTISE HERE