Uongozi wa Simba wawashangaa wanaodai Aveva ametelekezwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
11 Jan 2018
Uongozi wa Simba wawashangaa wanaodai Aveva ametelekezwa
Uongozi wa Simba umesema madai ya kwamba wamemtelekeza Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva aliyelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, hayana ukweli wowote.

Rais huyo wa Simba ambaye amekuwa mahabusu kutokana na kukabiliwa na kesi ya utakatishaji wa fedha, alipelekwa Hospitali ya Temeke, jijini na baadaye kuhamishiwa Muhimbili kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa figo.

Katika mahojiano na gazeti la michezo la Bingwa,Katibu Mkuu wa Simba, Dk. Anorld Kashembe, alisema kuna viongozi wa juu wa klabu yao walikwenda kumjulia hali na kwamba hawawezi kumtupa mwenzao huyo hasa katika kipindi hiki.

“Mimi nipo Arusha natarajia kurudi kesho(leo), lakini hizo taarifa zinazodai kuwa Rais (Aveva) ametelekezwa hazina ukweli wowote, kwani kuna viongozi ambao walikwenda kumjulia hali hospitalini na hali yake inaendelea vizuri,” alisema Kashembe.

Alisema miongoni mwa viongozi waliokwenda kumjulia hali Aveva ni Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ pamoja na Kaimu Makamu, Iddi Kajuna, ambao walithibitisha kuwa hali yake inaendelea kuimarika.

Aveva Jumapili ya wiki iliyopita alikimbizwa Hospitali ya Temeke baada ya hali yake kubadilika akiwa mahabusu katika Gereza la Keko, jijini kabla ya kuhamishiwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
46m ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →