Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema amepokea maelfu ya meseji kutoka kwa mashabiki wa Simba wakimtaka arejee kunako klabu hiyo
Aussems ambaye kwa sasa yuko mapumziko huko Ufaransa, ameeleza kuguswa na jumbe hizo kutoka kwa mashabiki wa Simba
Mbelgiji huyo amesema kuwa anaamini siku moja atarudi Simba
"Nimeguswa na maelfu ya meseji nilizopokea kutoka kwa mashabiki wakinitaka nirejee. Simba ni timu kubwa yenye wachezaji wazuri na mashabiki wa kipekee, nawatakia kila la kheri naamini tutakutana tena wakati mwingine," aliandika Aussems kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram
Tangu kuondoka kwa Mbelgiji huyo, timu imeonekana kupunguza kasi siku hadi siku chini ya kocha mpya Sven Vandenbroeck
Jana baada ya kufungwa na JKT Tanzania, mashabiki wa Simba walioshuhudia mchezo huo uwanja wa Uhuru, walikuwa wakiimba jina la Aussems wakiutaka uongozi wa Simba umrejeshe