Bocco afunguka kipigo dhidi ya JKT Tanzania

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Feb 2020
Bocco afunguka kipigo dhidi ya JKT Tanzania

Baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania, Nahodha wa Simba, John Bocco amesema walijichanganya na kuruhusu bao hilo huku nahodha wa JKT, Damas Mwakwaya akifunguka udhaifu walioonyesha Simba katika mchezo huo

Simba inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 50 imekubali kipigo hicho katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Uhuru ambapo wapinzani wao walifunga bao hilo pekee dakika ya 24 kipindi cha kwanza kupitia Adam Adam

Adam aliunganisha mpira wa krosi iliyochongwa na mchezaji mwenzake na kujaa wavuni licha ya kipa, Beno Kakolanya kujaribu kuchumpa kuucheza

Baada ya bao hilo, Simba ilipambana kusaka bao la kusawazisha na kukutana na kigingi kutoka kwenye ngome ya ulinzi ya JKT Tanzania.
Baada ya ya mchezo huo, Bocco aliwapongeza wapinzani wao kwa ushindi huo akibainisha kwamba walijichanganya na kuruhusu bao

"Baada ya kufungwa tulijaribu kupambana kupata matokeo lakini imelindikana, JKT walijipanga vizuri na wanastahili pongezi," alisema Bocco na kuongeza kwamba wanajipanga kwa ajili ya mechi zijazo

Nahodha na beki wa JKT Tanzania, Damas Makwaya alisema mpango walioingia nao umefanyakazi kwani wamepata matokeo mazuri waliyoyatarajia ambapo kabla ya kuingia uwanjani kocha wao Mohamed Abdallah 'Bares' aliwaelekeza jinsi ya kuwabana wapinzani wao.

"Alituelekeza tuwabane sana Simba, mpira ulivyoanza walikuwa kawaida, tukaona tuna uwezo wa kuwamudu na beki yao ilikuwa dhaifu," alisema na kuendelea

"Washambuliaji wetu walikuwa na kasi, hivyo tukatumia faida hiyo kusaka bao tumefanikiwa na kupata pointi tatu," alisema

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
16h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
16h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
19h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’