Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck leo atakiongoza kikosi chake kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting
Mchezo huo utapigwa saa kumi jioni kwenye uwanja wa Uhuru
Vandenbroeck yuko kwenye presha kubwa kutokana na mwenendo ambao timu imekuwa ikionyesha chini yake licha ya kupata matokeo
Inaelezwa mabosi wa Simba tayari wako mguu sawa kusaka mbadala wake kama mambo hayatabadilika
Mchezo wa leo dhidi ya JKT Tanzania unaweza kuwa mtihani wake wa kwanza, wanahitaji kuona Simba ikicheza vizuri na kupata ushindi
Matokeo tofauti na ushindi huenda yakapunguza siku zake za kuendelea kubaki kunako mabingwa hao wa nchi
Mbelgiji huyo leo anaweza kukirejesha dimbani kikosi kilichopata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union
Katika mchezo huo Simba ilitumia mfumo wa 4-4-2 ambao ulijumuisha washambuliaji wawili