Ibenge atajwa tena Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Feb 2020
Ibenge atajwa tena Simba

Kuna jambo linaweza kutokea Simba karibuni baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa viongozi wa mabingwa hao wa nchi wamewasiliana na Mkufunzi wa AS Vita Florent Ibenge

Mabosi wa Simba wanaweza kufanya mabadiliko mengine ya benchi la ufundi wakati wowote baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu chini ya kocha Sven Vandenbroeck

Ibenge ni miongoni mwa makocha ambao awali walikuwa wakiwaniwa na Simba kabla ya kumteua Vandenbroeck

Huyu ni kocha mwenye uzoefu mkubwa wa soka la Afrika. Ameiongoza AS Vita kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa au kombe la Shirikisho kila msimu aliokuwa kocha wa timu hiyo

Aliiongoza DR Congo kwenye michuano ya Afcon iliyofanyika mwaka jana nchini Misri, alijiuzulu baada ya michuano hiyo

Ibenge ni aina ya kocha ambaye timu yoyote inayohitaji mafanikio barani Afrika itamuhitaji

Pengine anaweza kuwa kocha anayefuata kunako klabu ya Simba, ni suala la muda tu

Tusubiri..

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
39m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’