Mabingwa wa nchi Simba wamekamilisha munguuko wa kwanza ligi kuu ya Vodacom wakijikusanyia alama 50 baada ya kushuka dimbani mara 19
Simba iko kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 12 dhidi ya Azam Fc ambayo inashika nafasi ya pili na alama 16 dhidi ya Yanga inayoshika nafasi ya tatu
Uongozi wa Simba umejiwekea malengo ya kutwaa ubingwa wa msimu huu kwa kufikisha angalau alama 100
Ni jambo ambalo halikuwahi kutokea miaka ya nyuma na kama vinara hao watafanikisha basi wataandika historia mpya
Hata hivyo ili kufanikisha malengo hayo, kocha Sven Vandenbroeck anapaswa kuwa makini kwani mechi za duru ya pili mara nyingi zinakuwa na ushindani zaidi
Hii ni kutokana na baadhi ya timu kuwa kwenye harakati za kujinusuru kuteremka daraja na msimu huu timu sita zitakuwa kwenye mchakato huo
Nne zitashuka moja kwa moja na mbili zitacheza play-off
Kwa upande wa mbio za ubingwa, Simba iko kwenye nafasi nzuri zaidi kwani pamoja na changamoto ndogondogo zinazoonekana, haitakuwa kazi rahisi mabingwa hao wa nchi kupoteza uongozi wa alama 12
Pengine ubingwa unaweza kutangazwa mapema sana Msimbazi na kubaki kufukuzia rekodi ya alama mia