Hakuna tofauti benchi la ufundi Simba - Senzo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Feb 2020
Hakuna tofauti benchi la ufundi Simba - Senzo

Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema hakuna tofauti yoyote kwenye benchi la ufundi la timu hiyo

Mazingisa ametoa kauli hiyo baada ya kuendelea kushamiri kwa tetesi kuwa Mkufunzi Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck hapikiki chungu kimoja na Kocha Msaidizi Selemani Matola pamoja na wataalam wengine wa benchi la ufundi

Senzo amesema sintofahamu hiyo inatengenezwa na vyombo vya habari tu kwani hajawahi kupokea malalamiko kutoka kwa kocha au viongozi wengine wa benchi la ufundi

"Malalamiko ya kutokuwepo maelewano kwenye benchi la ufundi hayapo, hakuna tatizo lolote, habari hizi tunazisikia kutoka kwenu (Wanahabari) lakini hakuna ukweli wowote," amesema Mazingisa

Aidha akizungumzia kiwango kinachoonyeshwa na Simba chini ya Sven, Mazingisa amekiri kuwepo mapungufu lakini amesema zipo sababu likiwemo suala la majeruhi

Amesema benchi la ufundi linaendelea kufanyia kazi changamoto hizo

Kumekuwa na taarifa kuwa uongozi wa Simba unaweza kuchukua uamuzi mgumu wa kuachana na Vandenbroeck baada ya kutoridhishwa na kiwango cha timu

Lakini pia inaelewa kocha huyo hana ushirikiano mzuri na makocha wenzake wa benchi la ufundi

Mmoja wa viongozi wa Simba amekiri kuwepo kwa tofauti hiyo ambapo Sven anatuhumiwa kutumia ubabe na lugha zisizo za kistaarabu kwa wasaidizi wake

Aidha Sven pia amekuwa hatoi ushirikiano kwa wanahabari, mara kwa mara akigoma kuzungumza nao wanapohoji masuala mbalimbali

Sven amekataa kufanya mahojiano ya wanahabari katika mazoezi ya Simba na hata mahojiano ya kabla ya mchezo

Ni tofauti na mtangulizi wake Patrck Aussems ambaye alitoa taarifa kwa wanahabari kuhusu mwenendo wa kikosi chake mara kwa mara

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
29m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’