Maoni na ukosoaji unaotolewa na mashabiki wa Simba licha ya timu yao kuendelea kupata ushindi ni ishara kuwa hawaridhishwi na kile wanachokiona
Ujio wa kocha Sven Vandenbroeck bado haujaonekana kuwa na manufaa na bahati mbaya zaidi amechukua majukumu kutoka kwa Mbelgiji mwenzie Patrick Aussems ambaye aliacha timu ikiwa kwenye kiwango bora
Simba ni klabu kubwa Tanzania, ina utamaduni na soka la kipekee, kushinda pamoja na kuwapa burudani mashabiki wake
Lakini kwa sasa mashabiki hawapati burudani waliyoizoea, na hata matokeo pia yanapatikana kwa taabu sana
Simba ina malengo makubwa sana, kwa sasa matarajio ya wengi ni kuona wanakuwa na timu imara ambayo itaweza kushindana na vigogo wa soka barani Afrka katika michuano ya ligi ya mabingwa
Lakini mpaka sasa mwelekeo hauonekani kuwa hivyo, Sven anapaswa kuchukua hatua haraka, anapaswa kuanzia pale alipoishia Aussems na sio kuanza upya
Kwani ni wazi timu inaonekana kushuka kiwango, timu pinzani zimeanza kuondoa hofu zinapokutana na Simba
Ukiangalia walivyocheza Polisi Tanzania jana, hawakuigopa kabisa Simba, walionekana bora kila idara
Kumekuwa na malalamiko juu ya mfumo wa mshambuliaji mmoja anaotumia, lakini pia uchaguzi wa wachezaji kulingana na mechi bado ni changamoto
Wengi wanajiuliza kikosi cha kwanza cha Simba ni kipi? maana pamoja na kufanya 'rotation' ya wachezaji, lazima timu iwe na kikosi cha kwanza
Baadhi ya wachezaji wanaonekana kushuka viwango, hapa linakuja suala la jinsi wanavyoandaliwa mazoezini
Sven ana bahati ya kufanya kazi na kocha msaidizi Selemani Matola, ambaye analifahamu vyema soka la Tanzania na pia anawafahamu vizuri wachezaji wengi wa Simba
Sidhani kama anamtumia vizuri