Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amewapongeza wachezaji wa timu hiyo kwa upambanaji walioonyesha kwenye kipindi cha pili na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania
Mbelgiji huyo amesema mabadiliko waliyofanya kwenye kipindi cha pili yaliwarejesha mchezoni na muhimu zaidi wachezaji walifahamu wanahitaji kupata matokeo
"Ukiangalia kipindi cha kwanza hatukucheza vizuri, hatukuwa bora kwenye safu ya kiungo Polisi Tanzania walituzidi. Lakini ni kawaida unapocheza kila baada ya siku mbili, kipindi cha pili timu inakuwa sawa. Nawapongeza wachezaji wangu kwani ni mara ya nne hii tunalazimika kutokea nyuma kupata ushindi," alisema
Nae kocha wa Polisi Tanzania Malale Hamsini amesema timu yake ilicheza vizuri na walikuwa na kila sababu ya kupata ushindi lakini suala la kukosa uzoefu kwa baadhi ya wachezaji limewagharimu