Mabingwa wa nchi Simba wameendeleza umwamba wao uwanja wa Taifa baada ya kuilaza timu ngumu ya Polisi Tanzania mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu uliopigipwa kwenye dimba hilo
Polisi Tanzania ilitawala mchezo huo kipindi cha kwanza na walifanikiwa kufunga bao la kuongoza kupitia Sixtus Sabilo, bao lililowapeleka mapumziko wakiwa wako mbele
Hata hivyo kipindi cha pili Simba ilirejea ikiwa imara na kufanikiwa kusawazisha bao hilo kwenye dakika ya 57 kupitia kwa nahodha John Bocco aliyefungeua akaunti yake ya mabao msimu huu

Wakati mchezo huo ukionekana kama ungemalizika kwa sare Ibrahim Ajib Migomba aliwapa furaha mashabiki wa Simba ikifunga bao la ushindi kwenye dakika za lala salama
Kwa mara nyingine tena, Simba imetumia uzoefu kuweza kupata ushindi katika mchezo ambao kwa nyakati tofauti walikuwa na wakati mgumu
Ushindi huo unaifanya Simba ikamilishe duru ya kwanza ikifikisha alama 50