Fraga ampagawisha Mgunda

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Feb 2020
Fraga ampagawisha Mgunda

kufunzi wa timu ya  Coastal Union, Juma Mgunda, amesema kiungo mkabaji wa Simba, Mbrazil Gerson Fraga, ndiye aliyemvutia kwa kucheza kandanda safi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo huo uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Simba walishinda mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union, mabao yote yakifungwa na Fraga.

Mgunda amemtaja Fraga kuwa ni mchezaji anayeyajua majukumu yake, lakini pia ana akili ya mpira.

"Nimevutiwa sana na Mbrazil yule wa Simba , ana uwezo mzuri wa kupanda na kushuka kwa wakati, msumbufu, mbabe na si mwoga wa kufanya jambo"

"Ukiwa na wachezaji kama hawa watatu katika kikosi chako una uhakika wa kupata matokeo ya ushindi kwa sababu  wanaonyesha kuwa na kiu ya kufanya jambo," Mgunda amenukuliwa na gazeti la Bingwa

Mgunda alisema kama anatamani nyota huyo angekuwa ndani ya kikosi chake kwa sababu angesaidia kuwabadili wachezaji wake kutokana na changamoto ambayo angeitoa.

"Nimevutiwa naye sana na natamani kama angekuwa kikosi kwangu kupitia yeye wachezaji wengine wangebadilika kwa sababu anaonyesha wazi kuna kitu anakihitaji uwanjani na ndio maana si mwoga kwa kila kitu."

Fraga alifunga mabao yote mawili ya Simba kwenye mchezo huo

Jumla ameishaifungia Simba ambao manne kwenye mashindano yote tangu alipojiunga na mabingwa hao wa Tanzania Bara mwezi Juni 2019

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
20m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
18h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
21h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE β†’