Samatta atoa ombi maalum kwa mashabiki wa soka, Manara atia neno

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Feb 2020
Samatta atoa ombi maalum kwa mashabiki wa soka, Manara atia neno

Mshambuliaji wa Aston Villa Mbwana Samatta amewaomba mashabiki wa soka nchini kuacha kutukana kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za klabu yake hiyo pamoja na kurasa za wachezaji wenzake

Samatta amekuwa mchezaji wa kwanza Mtanzania kucheza ligi kuu ya Uingereza huku akifanikiwa kufunga bao katika mchezo wake wa kwanza mwishoni mwa wiki dhidi ya Bournemouth

Hata hivyo kumejitokeza mashabiki Watanzania ambao wameingia kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya baadhi ya wachezaji wa Aston Villa wakiwatuhumu kumnyima pasi nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania

Samatta ameeleza kutofurahishwa na kitendo hicho akiwasihi waache tabia hiyo

Naye Afisa Habari wa Simba Haji Manara amewataka mashabiki wa soka nchini kuacha tabia hiyo kwani wanaweza kumharibia Samatta

"Watanzania nawasihi sana kama mnampenda Samata na kumtakia kheri katika maisha yake huko Aston Villa,tuache kutukana na kuongea maneno ya hovyo kwa wachezaji wenzie na klabu yake kwa ujumla!!"

"Msidhani kufanya hvyo ndio kumpenda Champion boy,ni kumweka katika presha ambayo hastahiki kwa sasa,,
Mnakosea sana na sasa tuanze kukemeana huu upuuzi tunaoupeleka kule"

"Grealish hawezi kumnyima pasi Samata kusudi kwa sababu yoyote ile,,level ya professional player hawafanyi ujinga ujinga huo,,na kuendelea kumtukana Nyota huyo wa Villa na captain wao ni kumweka mwenzetu katika hali ngumu klabuni!!"

"Kiukweli tunafanya ushamba mkubwa na inaonyesha ulimbukeni wetu Wabongo!!"

"Kiufupi social media hatuitendei haki Watanzania wengi na hz Abuse kwa wazungu msidhani wanachukulia tunavyochukulia sie,mnaotutukana kila siku!!"

"Wote tushiriki kumsaidia mchezaji wetu bila kumtengenezea mazingira magumu katika kazi yake inayoitangaza nchi"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’