Kwa mara ya kwanza juzi kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union, mkufunzi wa Simba Sven Vandenbroeck aliwatumia pamoja washambuliaji John Bocco na Meddie Kagere
Yalikuwa ni mabadiliko ya mfumo kutoka 4-3-3 na kuwa 4-4-2, mfumo ambao kwa kiasi kikubwa uliipa Simba uwiano mzuri kwenye kujilinda na kushambulia
Ni katika mchezo huo Simba ilifanikiwa kuondoka na 'cleansheet' baada ya kushindwa kufanya hivyo katika michezo saba mfululizo
Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 ambayo yote yalifungwa na kiungo mkabaji raia wa Brazil Gerson Fraga
Pengine Vandenbroeck ataendelea na mfumo huo katika mchezo unaofuata dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa kesho Jumanne kwenye uwanja wa Taifa
ADVERTISE HERE