Mabingwa wa nchi Simba kesho Jumanne wataendeleza burudani kwenye uwanja wa Taifa watakapoikabili Polisi Tanzania kwenye mchezo wa kukamilisha mzunguuko wa kwanza ligi kuu ya Vodacom
Ushindi kwa Simba utawafanya wafikishe alama 50 na hivyo kumaliza duru ya kwanza wakipoteza alama saba tu
Mpaka sasa Simba wanaongoza ligi wakiwa wamejikusanyia alama 47 baada ya kushuka dimbani mara 18
Simba ndio timu pekee iliyopoteza mchezo mmoja tu na kutoka sare mara mbili. Inaongoza ligi kwa tofauti ya alama 10
Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema wanahitaji kutumia vyema uwanja wa nyumbani kwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo
Β
ADVERTISE HERE