Ubingwa kwanza, kiatu baadae - Kagere

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Feb 2020
Ubingwa kwanza, kiatu baadae - Kagere

Mshambuliaji kinara wa mabao kwenye kikosi cha Simba Meddie Kagere amesema tuzo ya mfungaji bora msimu huu sio kipaumbele kwake muhimu anataka kuisaidia Simba kutwaa taji 21 la Ligi Kuu Bara.

Simba imetwaa mataji 20 ya ligi ikiachwa kwa mataji saba na wapinzani wao Yanga wenye mataji 27, endapo watafanikiwa kulitwaa msimu huu watabakiza deni la mataji sita tu

Msimu wake wa kwanza akiwa na Simba 2018/19, Kagere alifunga mabao 23 katika ligi na timu yake ilitwaa kombe kwa mara ya pili mfululizo ikimaliza na pointi 93, huku ikifunga mabao 77

Mpaka sasa Kagere amefunga mabao 12, akihitaji kufunga mabao 11 katika mechi 20 zilizobaki ili kufikia rekodi yake ya msimu uliopita

"Nafasi yangu na kazi yangu inaniruhusu kufunga na kutengeneza mabao, ninamshukuru Mungu kwa hili, mashabiki pia nawashukuru kwa kuwa wananipa sapoti, nitazidi kupambana ili kuhakikisha tunatetea ubingwa mara ya tatu" alisema Kagere

"Sifikirii sana ufungaji bora, jambo kubwa kwangu na kwa wachezaji wote wa Simba ni kuhakikisha tunatwaa ubingwa ili tupate nafasi ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao"

Mpaka sasa Simba iko kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa kwake licha ya kuwa bado ni mapema, inaongoza ligi ikiwa imejikusanyia alama 47, alama 10 zaidi ya Azam Fc inayofuata nafasi ya pili

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’