Kiungo wa Simba raia wa Brazil Gerson Fraga amesema kuwa anajisikia faraja kufunga mabao yote kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union jana
Fraga alifunga mabao yote mawili kwenye ushindi wa 2-0 ambao Simba ilipata dhidi ya Coastal Union kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa
"Ni jambo la furaha sana kwangu kuweza kuifungia Simba mabao mawili na kuisaidia kupata ushindi. Nimefurahi kutimiza wajibu wangu baada ya kupewa nafasi na kocha," alisema
"Pia nimefarijika kuwapa furaha mashabiki wetu ambao wanatupa upendo na kutuunga mkono kwa kuja uwanjani kwenye michezo yetu"
Aidha akizungumzia ufinyu wa nafasi anayopata kwenye kikosi cha kwanza, Fraga amesema atahakikisha anatimiza wajibu wake kila atakapopewa nafasi lakini pia atawaunga mkono wachezaji wengine wanaopewa majukumu ya kuanza kwenye timu
Tangu ajiunge na Simba mwezi Julai, Fraga amefunga mabao manne, matatu kwenye ligi na moja kwenye kombe la FA