Wachezaji wapya wa Simba Shiza Kichuya na Luis Miquissone huenda wakaanza kuwatumikia mabingwa hao wa nchi baada ya maombi ya vibali vyao kufanikiwa
Juzi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' alitembelea Makao Makuu ya FIFA huko Uswisi ambapo pamoja na mambo mengine alifanya mazungumzo na Rais wa FIFA Gianni Infantino
Simba iliwasilisha maombi FIFA ikiomba ipatiwe kibali cha muda ili kuweza kumtumia Miquissone ambaye kuna mvutano kati ya vilabu vya UD Songo na Mamelodi Sundowns
Sundowns walimuuza Miquissone kwa Simba wakati akitokea kwa mkopo klabu ya UD Songo
Aidha kuhusu kibali cha Kichuya inaelezwa FIFA imekiagiza chama cha soka cha Misri kitoe kibali chake jambo ambalo inaelezwa limekamilishwa hata hivyo klabu ya ENPPI bado inadai kummiliki mchezaji huyo