Kufuatia mwenendo usioridhisha wa safu ya ulinzi ya Simba ambayo imeruhusu bao kwenye kila mchezo katika michezo saba iliyopita, kocha mkuu wa mabingwa hao wa nchi Sven Vandenbroeck anatarajiwa kufanya mabadiliko ya safu yake kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Coastal Union
Mchezo huo wa ligi kuu utapigwa kwenye uwanja wa Taifa
Juzi mkongwe Paschal Wawa alipata majeraha ambayo huenda yatamuweka nje kwa wiki kadhaa
Tairone Da Silva raia wa Brazil huenda akachukua nafasi yake huku Kennedy Juma akitajwa kuwa anaweza kuchukua nafasi ya Erasto Nyoni
Mashabiki wamtaka Mlipili
Aidha baadhi ya mashabiki wa Simba wamehoji alipo beki Yusufu Mlipili ambaye msimu huu hajacheza mchezo wowote wa kimashindano
"Viongozi watuambie Mlipili yuko wapi? Maana haiwezekani tunaona safu ya ulinzi haiko sawa lakini nje kuna wachezaji ambao tunaamini kama wakipewa nafasi wanaweza kufanya vizuri, lakini hawatumika," alisema Sudi Mnyama mdau mkubwa wa klabu ya Simba
Simba imeshinda mechi nne zilizopita lakini kumekuwa na makosa mengi yanayofanyika kwenye safu ya ulinzi ambayo yanapelekea kuruhusu mabao mepesi