Jana kinara wa mabao ligi kuu Meddie Kagere aliendeleza moto wake wa kutupia kambani akifunga bao muhimu ambalo liliipa Simba ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Namungo Fc
Utamu wa bao hilo unatokana na muda ambao limefungwa, dakika ya 89'
Bao hilo ni kama limepeleka kilio upande wa pili kwani wao ndio wanaolalamika zaidi kuliko Namungo Fc!
Sasa amefikisha mabao 12 akiendelea kujikita kileleni kwenye mbio za kuwania kiatu cha dhahabu
Anaongoza kwa tofauti ya mabao matano dhidi ya wachezaji wengine wanaomfuatia
Msimu uliopita aliibuka mfungaji bora na mabao yake 23, msimu huu ameahidi kuvunja rekodi yake aliyoweka msimu uliopita kwa kufunga mabao zaidi ya 23
Bado ana michezo 21 kufanikisha lengo hilo
Β
ADVERTISE HERE