Simba vs Namungo Fc kupigwa uwanja wa Taifa leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Jan 2020
Simba vs Namungo Fc kupigwa uwanja wa Taifa leo

Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo Jumatano, Januari 29 2020 kitashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Namungo Fc katika mchezo wa ligi

Mchezo huo utapigwa kuanzia saa moja jioni

Vinara hao wa ligi kuu wamepania kuondoka na alama zote tatu ili kuendelea kujikita kileleni kwa kufikisha alama 44

Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema wamefanya maandalizi ya kutosha na wana matumaini makubwa ya kushinda mchezo huo

Namungo Fc iliyopanda daraja msimu uliopita, imekuwa na msimu mzuri ikiwa inshika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi na alama zao 28

Timu hiyo inafundishwa na kocha raia wa Burundi, Hitimana Thierry

Jana Namungo Fc ilipata udhamini wa Sportpesa baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Tsh Milioni 120

Hata hivyo watakutana na Simba ambayo iko kwenye kiwango kizuri ikitoka kushinda michezo mitatu mfululizo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
12h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’