Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa beki wa kulia wa Simba Shomari Kapombe
Kapombe ameitumia siku hii kuwakumbuka wazazi wake ambao wote wametangulia mbele ya haki
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram Kapombe ameandika ujumbe huu;
"Leo ni siku nyingine muhimu ya kuzaliwa.Mungu awarehem wazazi wangu waliotangulia mbele ya haki"
"Pumzika kwa amani Mzee Salum ikiwa nimekushuhudia tu kwenye picha kuna muda natamani ungekuwepo maana ya duniani yananizid na sina wa kumkimbilia"
"Mungu akurehem mzee wangu huwa nafarijika ninaposimuliwa juu ya uwezo uliokuwa ukionyesha uwanjani huwa naenjoy na nafurahi kurithi no 2 kutoka kwako"
"Pumzika kwa Amani mama yangu kipenzi uliniacha na miaka 10 ulikuwa mama bora kwangu ,nakupenda sana na yote uliyonihusia niliyafata na kuyazingatia hakika ni mtoto mwema ninayepitia magumu"
"Nakupenda sana mama uliniacha mikono salama kwa mama yako mzazi aliyenilea vyema sana ila na yeye Mungu alimpenda zaidi"
"Pumzika bibi yangu kipenzi wewe uliyenifanya mimi kufika hapa leo hii"
"Niliombewa na kupakwa upako wa mgonjwa kwa mara ya mwisho lakini uliamini ninayo nafasi duniani siku ya tatu baadae niliamka ndipo nikabatizwa kwa jina la EMMANUEL MUNGU PAMOJA NAMI"
"Mungu awape kauli thabiti nawapenda sana wapendwa wangu"
Familia ya Wanamsimbazi tunakupa pole sana kwa mapito uliyopitia, tunakutakia siku njema ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwako
Happy BirthDay Shomari Kapombe..