Sven kuja na mkakati wa kutetea ubingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Jan 2020
Sven kuja na mkakati wa kutetea ubingwa

Mkufunzi wa Simba Sven Vanderboeck amesema licha ya kikosi chake kuongoza ligi, wanahitaji kupambana kuhakikisha wanabaki kileleni kutokana na ushindani kuongezeka

Simba inaongoza ligi ikiwa imekusanya alama 41 baada ya kushuka dimbani mara 16. Inaongoza kwa tofauti ya alama sita dhidi ya Azam Fc yenye alama 35

Vandenbroeck ana miezi miwili tangu atue Tanzania, hadi sasa ameingoza Simba kwenye mechi za ligi dhidi ya Lipuli FC, KMC, Ndanda, Yanga, Mbao na Alliance huku akivuna pointi 16, akishinda mechi tano na sare moja.

Mbelgiji huyo amesema anauona ugumu mkubwa kwa sababu kila timu wanayocheza nayo inacheza kwa kujituma kutaka kupata pointi huku suala la ratiba likiwa changamoto pia

β€œUnajua wakati nakuja hapa nilifikiri kila kitu kitakuwa rahisi tu lakini nimegundua ni tofauti kabisa. Ligi ni ngumu sana kwa sababu kila timu ambayo tunacheza nayo inacheza zaidi ya ule uwezo wao kwa ajili ya kutuzuia," amesema

"Lakini pia nimegundua ukicheza na hizi timu ambazo zinaonekana ndogo ushindani huwa mkubwa sana na ndiyo maana kama umeangalia inakuwa hatuna ushindi mkubwa sana kwao, tunashinda kwa mabao machache mno"

"Kitu kingine ambacho kinaongeza hali hiyo ni kukosekana kwa muda mrefu wa kupumzika kutokana na ratiba yetu ilivyo," Sven amenukuliwa na gazeti la Sport Xtra

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
10h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’