Mkufunzi wa Simba Sven Vanderboeck amesema licha ya kikosi chake kuongoza ligi, wanahitaji kupambana kuhakikisha wanabaki kileleni kutokana na ushindani kuongezeka
Simba inaongoza ligi ikiwa imekusanya alama 41 baada ya kushuka dimbani mara 16. Inaongoza kwa tofauti ya alama sita dhidi ya Azam Fc yenye alama 35
Vandenbroeck ana miezi miwili tangu atue Tanzania, hadi sasa ameingoza Simba kwenye mechi za ligi dhidi ya Lipuli FC, KMC, Ndanda, Yanga, Mbao na Alliance huku akivuna pointi 16, akishinda mechi tano na sare moja.
Mbelgiji huyo amesema anauona ugumu mkubwa kwa sababu kila timu wanayocheza nayo inacheza kwa kujituma kutaka kupata pointi huku suala la ratiba likiwa changamoto pia
βUnajua wakati nakuja hapa nilifikiri kila kitu kitakuwa rahisi tu lakini nimegundua ni tofauti kabisa. Ligi ni ngumu sana kwa sababu kila timu ambayo tunacheza nayo inacheza zaidi ya ule uwezo wao kwa ajili ya kutuzuia," amesema
"Lakini pia nimegundua ukicheza na hizi timu ambazo zinaonekana ndogo ushindani huwa mkubwa sana na ndiyo maana kama umeangalia inakuwa hatuna ushindi mkubwa sana kwao, tunashinda kwa mabao machache mno"
"Kitu kingine ambacho kinaongeza hali hiyo ni kukosekana kwa muda mrefu wa kupumzika kutokana na ratiba yetu ilivyo," Sven amenukuliwa na gazeti la Sport Xtra