Simba inayoji-mwambafai kwa kuwa na viungo bora

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Jan 2020
Simba inayoji-mwambafai kwa kuwa na viungo bora

Wakati wa usajili wa dirisha dogo, kulikuwa  na maoni, mapendekezo na ushauri kutoka kwa mashabiki wa Simba ambao walikuwa wakitaka mabingwa hao wa nchi wasajili mshambuliaji hasa baada ya kuachana na Mbazil Wilker Da Silva

Hata hivyo Simba iliongeza viungo wawili Shiza Kichuya na Luis Miquissone ambao bado wanasubiri ITC zao kabla ya kuanza majukumu

Lakini kwa wastani, viungo wa klabu hiyo wamekuwa wakifanya vizuri

Kwani wanahusika kwenye kufunga mabao lakini pia kutengeneza nafasi za mabao

Francis Kahata na Clatous Chama ndio vinara wa mabao upande wa viungo wakiwa wamefunga mabao matano kila mmoja huku wakitengeneza mabao matatu

Hassan Dilunga amefunga mabao manne huku akitengeneza nafasi mbili za mabao wakati Sharaff Shiboub amefunga mabao mawili lakini ametoa pasi tano za mabao

Jonas Mkude na Gerson Fraga wamefunga mabao mawili kila mmoja wakati Ibrahim Ajib amefunga bao moja lakini ametoa pasi tano za mabao

Viungo hao Wamehusika moja kwa moja katika mabao 40 kwenye mechi za Ligi na Kombe la Shirikisho Azam

Pengine hii inaweza kuwa sababu kwa nini uongozi wa Simba haukuona umuhimu wa kuongeza mshambuliaji kwani uwepo wa Meddie Kagere. Miraji Athumani, John Bocco pamoja na viungo hawa ni silaha tosha kutetea ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa tatu mfululizo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
13h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
16h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
22h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’