Wakati wa usajili wa dirisha dogo, kulikuwa na maoni, mapendekezo na ushauri kutoka kwa mashabiki wa Simba ambao walikuwa wakitaka mabingwa hao wa nchi wasajili mshambuliaji hasa baada ya kuachana na Mbazil Wilker Da Silva
Hata hivyo Simba iliongeza viungo wawili Shiza Kichuya na Luis Miquissone ambao bado wanasubiri ITC zao kabla ya kuanza majukumu
Lakini kwa wastani, viungo wa klabu hiyo wamekuwa wakifanya vizuri
Kwani wanahusika kwenye kufunga mabao lakini pia kutengeneza nafasi za mabao
Francis Kahata na Clatous Chama ndio vinara wa mabao upande wa viungo wakiwa wamefunga mabao matano kila mmoja huku wakitengeneza mabao matatu
Hassan Dilunga amefunga mabao manne huku akitengeneza nafasi mbili za mabao wakati Sharaff Shiboub amefunga mabao mawili lakini ametoa pasi tano za mabao
Jonas Mkude na Gerson Fraga wamefunga mabao mawili kila mmoja wakati Ibrahim Ajib amefunga bao moja lakini ametoa pasi tano za mabao
Viungo hao Wamehusika moja kwa moja katika mabao 40 kwenye mechi za Ligi na Kombe la Shirikisho Azam
Pengine hii inaweza kuwa sababu kwa nini uongozi wa Simba haukuona umuhimu wa kuongeza mshambuliaji kwani uwepo wa Meddie Kagere. Miraji Athumani, John Bocco pamoja na viungo hawa ni silaha tosha kutetea ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa tatu mfululizo