Nyota wa zamani wa mpira wa kikapu Kobe Bryant (41) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika ajali ya chopa
Ajali hiyo pia imemuondoa duniani binti yake wa miaka 13 Gigi pamoja na watu wengine saba
Mamlaka za usalama nchini Marekani zinafanya jitihada za kuinasua miili ya wahanga

Chanzo cha ajali hiyo imeelezwa kuwa ni hali ya ukungu iliyopelekea chopa hiyo kupoteza mwelekeo na kuanguka milimani
Dunia imepokea kifo cha mkongwe huyo wa LA Lakers kwa mshituko mkubwa kutokana na mchango wake kwenye mchezo wa mpira wa kikapu katika miaka 20 aliyocheza
Pamoja na kuwa gwiji wa mpira wa kikapu, Kobe alishiriki shughuli nyingi za kijamii
Mungu ailaze roho yake mahali pema, AMEN
ADVERTISE HERE