Vandenbroeck akerwa na safu ya ulinzi Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Jan 2020
Vandenbroeck akerwa na safu ya ulinzi Simba

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema wanahitaji kufanyia kazi mapungufu yanayojitokeza kwenye safu ya ulinzi ili kuhakikisha hawaruhusu mabao kizembe

Mbelgiji huyo ametoa kauli hiyo jana baada ya mchezo wa raundi ya nne kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Mwadui Fc, mchezo ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1

Katika michezo ya hivi karibuni safu ya ulinzi imekuwa ikiruhusu wastani wa bao moja kwenye kila mchezo

Waliruhusu mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Yanga, wakaruhusu mabao mawili kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi na pia wameruhusu mabao matatu kwenye michezo mitatu iliyopita

"Tunaruhusu mabao mepesi, sio jambo jema. Tuna tatizo katika kujipanga na mawasiliano. Tutafanyia kazi changamoto hiyo ingawa hatuna muda wa kutosha kutokana na kuwa na mechi nyingi katika kipindi cha siku tisa zijazo," alisema Vandenbroeck

Akizungumzia mchezo huo, Vandenbroeck alisema timu yake iliicheza vizuri pamoja na kukabiliwa na changamoto za hapa na pale

Aidha Vandenbroeck ameongeza program za mazoezi kwa wachezaji wake baada ya kubaini kuna changamoto ya utimamu wa mwili kwa baadhi ya wachezaji

Jana baada ya mchezo dhidi ya Mwadui Fc ambao ulipigwa uwanja wa Taifa, wachezaji walibaki dimbani hapo kuendelea na mazoezi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’