Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wamesonga mbele michuano ya kombe la Azam (ASFC) baada ya kuichapa Mwadui Fc mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa
Kwa mara nyingine, licha ya kutokea nyuma kwa bao moja, wachezaji wa Simba walipambana kuweza kuibuka na ushindi huo
Mathias Mdamu aliitanguliza Mwadui Fc kwenye dakika ya 35 kabla Clatous Chotta Chama 'CCC' kuisawazishia Simba kwa bao murua sana kwenye dakika ya 45
Kipindi cha pili Simba iliendelea kutawala mchezo huku Mwadui FC wakitumia zaidi mashambulizi ya kushitukiza
Alikuwa ni Francis Kahata aliyeihakikishia Simba ushindi huo maridhawa kwa kufunga bao muhimu kwenye dakika ya 85
Ushindi huo ni kama Simba imelipa kisasi cha kipigo cha bao 1-0 waichofungwa na Mwadui Fc kwenye mchezo wa ligi kuu