Simba kuandika barua FIFA kudai vibali vya Miquissone, Kichuya

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Jan 2020
Simba kuandika barua FIFA kudai vibali vya Miquissone, Kichuya

Uongozi wa klabu ya Simba unafikiria kuandika barua kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kuomba usaidizi ili kupata ITC za wachezaji wapya Shiza Kichuya na Luis Miquissone

Inaelezwa vyama vya soka vya Msumbiji na Misri vimeweka ngumu kutoa vibali vya nyota hao

Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema kumekuwa na ugumu kupata ITC za wachezaji hao lakini hawafahamu tatizo liko wapi hivyo kama italazimu wataomba usaidizi wa FIFA ikiwezekana wapewe vibali vya muda ili wachezaji waanze kucheza

"Luis na Kichuya wote wana tatizo moja ambalo ni kutopata ITC, kibali cha Luis kipo Msumbuji wakati Kichuya kipo Misri. Kuna mabishano kadhaa kwa pande za FA na klabu zao walizokuwa wakizichezea hivyo, tunataka kuiomba Fifa watupe vibali vya muda ili tuweze kuwatumia wachezaji hao wakati mengine yanaendelea.

"Hatufahamu tatizo hasa ni nini, kama ni ishu ya kimkataba ama la, ndiyo maana tunataka kwenda Fifa, ambapo pengine tutapata ufumbuzi na kujua tatizo. Kwa upande wetu tunafanyia kazi mchakato huu maana yote ni sahihi ingawa wachezaji wanachelewa kuanza kucheza,” Senzo amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

Hata hivyo mapema jana Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu alisema ITC ya Kichuya tayari imewasili na anaweza kucheza mchezo dhidi ya Mwadui Fc hapo kesho kama kocha Sven Vandenbroeck atampa nafasi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’