Simba hatarini kumkosa Wawa kwa mechi tatu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Jan 2020
Simba hatarini kumkosa Wawa kwa mechi tatu

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mguto, amesema beki kisiki wa Simba Pascal Wawa amepelekwa katika kamati ya maadili ya Shirikisho la Soka (TFF), kutokana na madai ya kumfanyia madhambi ya makusudi mshambuliaji wa Yanga, Ditram Nchimbi.

Wawa inadaiwa kufanya tukio hilo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliozikutanisha timu za Simba na Yanga Januari 4, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa video inayosambaa inaonyesha katika mchezo ule Wawa alimkanyanga Nchimbi  jambo ambao si la kiungwana katika soka.

Mguto amsema kwa sababu suala hilo halikuwapo katika ripoti ya mwamuzi wala  kwa kamisaa wa mchezo,  lakini video yake mtandaoni  inazua gumzo.

 “Katika kamati hiyo wataiangalia na kuona kama kilikuwa kitendo cha makusudi au laa,  lakini pia watatushauri kamati ya uendeshaji wa ligi jambo gani la kufanya.

“Hatuionei timu yoyote kwetu Simba, Yanga na timu nyingine zote tunazisimamia kwa usawa hatuwezi kupendelea upande mmoja,”

 Mguto alisema: “Bila shaka suala la madhambi yaliofanywa na Wawa litamalizika hivi karibuni kwa sababu tayari video ya tukio zima tunayo na kuiwasilisha sehemu husika, ” Mguto alinukuliwa na gazeti la Bingwa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’