Kikosi cha Simba kimewasili jijini Dar es Salaam leo kikitokea Zanzibar walipokuwa wakishiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi.
Kurejea kwa Simba kunatokana na timu hiyo kutupwa nje ya mashindano hayo wakiishia katika hatua ya makundi baada ya kufungwa jana bao 1-0 na URA ya Uganda.
Mara baada ya kuwasili na boti ya Azam majira ya saa saba mchana Simba walitawanyika katika makundi tofauti ambapo kocha wao mkuu Masoud Djuma aliondoka na usafiri wa basi la timu na baadhi ya wachezaji huku wengine wakichukua usafiri binafsi.
Hata hivyo mara baada ya timu hiyo kuwasili Djuma pamoja na wachezaji wake waligoma kuongea chochote na waandishi wa habari na kukimbilia kwenye basi lao.
Baada ya kuondoshwa kwenye michuano hiyo Simba inahamishia nguvu zake kwenye michuano ya ligi kuu ya Vodacom pamoja maandalizi ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

ADVERTISE HERE