Simba vs Mwadui Fc, mchezo wa kisasi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Jan 2020
Simba vs Mwadui Fc, mchezo wa kisasi

Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kesho Jumamosi Januari 25 2020 kitashuka kwenye uwanja wa Uhuru kuikabili Mwadui Fc katika mchezo wa raundi ya nne michuano ya kombe la Azam (ASFC)

Simba ilianza mazoezi juzi kujiandaa na mchezo huo baada ya kurejea kutoka mkoani Mwanza walikoshinda michezo miwili ya ligi dhidi ya Mbao Fc na Allliance Fc

Ni mchezo ambao Simba itakuwa nyumbani, ina kila sababu ya kuibuka na ushindi ili kutinga raundi ya tano ya michuano hiyo ambayo ni hatua ya 16 bora

Lakini pia huu utakuwa mchezo wa kisasi kwa Simba kwani Mwadui Fc ndio timu pekee liyopata ushindi dhidi ya Simba kwenye ligi

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema kikosi chake kinajiandaa kikamilifu ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi ili kutinga hatua inayofuata

Simba inayoendelea kujifua katika uwanja wake wa Mo Simba Arena, itaingia kwenye mchezo huo huku ari ya wachezaji wake ikiwa juu baada ya ushindi wa michezo miwili iliyopigwa jijini Mwanza

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’