Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa anatarajiwa kuweka hadharani hatma ya vibali vya kiungo mshambuliaji Luis Miquissone ambaye mpaka sasa bado hajaanza kuwatumikia mabingwa hao wa nchi
Miquissone na Shiza Kichuya walitua usajili wa dirisha dogo lililofungwa Januari 15 2020
Wakati ikielezwa kuwa ITC ya Kichuya imewasili, hali ni tofauti kwa Miquissone ambaye licha ya kusajiliwa mapema, bado kuna utata wa kupata ITC yake
Simba imemsajili Miquissone kutoka klabu ya Mamelodi Sundowns mabingwa wa Afrika Kusini hata hivyo mchezaji huyo aliitumikia kwa mkopo klabu ya UD Songo ya Msumbiji
ADVERTISE HERE