Pamoja na kuwa kadi za mashabiki zinazotolewa na klabu ya Simba kwa kushirikiana na benki ya Equity zitainufaisha timu hiyo, lakini uongozi wa Simba unahitaji kupanua wigo wa upatikanaji wa kadi hizo kote nchini
Lengo la Simba ni kutoa kadi angalau laki moja kwenye awamu yakwanza, lakini lengo hilo litafanikiwa haraka kama upatikanaji wa kadi utakuwa rahisi
Benki ya Equity ambayo imeingia ubia na Simba inapatikana katika miji mikubwa hivyo kuwanyima fursa mashabiki wengi ambao hawaishi katika miji hiyo
Hapa Simba na Equity wanapaswa kuweka Mawakala katika maeneo yote nchini ili kurahisisha upatikanaji wa kadi
Mashabiki wa Simba wameonesha utayari wa kumilikia kadi hizo baada ya kupewa elimu na kufahamu faida zake
Inatarajiwa baada ya uzinduzi ambao utafanyika Bungeni Dodoma Januari 29, kadi hizo zitasambazwa katika maeneo mengi zaidi